Goma: Bwana Bukye Mutehofu Jean anena kuwa hali yafanana shwari katani Mabanga ya kusini

Exif_JPEG_420

Akihojiwa na mwandishi habari wa la ronde info hîi juma nne tarehe 7 mei 2024, kiongozi makamu wa kata Mabanga ya kusini Bukye Mutehofu Jean anena kwamba raia wa eneo lake wanachapa kazi za maendeleo humo. Ijapo watu wamoja wakijiruhusha kujenga barabarani. Upande wa usalama hali yafanana kuwa shwari ijapo watu wenyi nia mbaya wajitokeza wakiiba ndani ya kata, baadae hunyatuka upande wa kempi ya askari jeshi Katindo2.

<< Sisi tuna hamasisha raia kuhusu kazi za maendeleo barabani. Tukifanya kazi za salongo kila juma mosi. Pamoja na raia tunajikaza kwa kuzibua tundu hapa na pâle barabarani zinazo pokea maji, kwa kuweka mawe>>, anena kiongozi makamu. Akiongeza kwamba watu wengine wenyi nia mbaya hujenga ndani ya barabara wakizuia kazi za maendeleo kufanyika vizuri.

Kuhusu usalama ndani ya kata kiongozi anena kwamba yafanana kuwa shwari, kwa kuwa watu wajitokeza mara kwa mara na kuiba ndani ya kata. Wanaposikia malalamiko hunyatuka wakijielekeza upande wa kempi ya askari jeshi Katindo2.

Kwa hiyo, kiongozi makamu wa kata Mabanga ya kusini Bukye Mutehofu Jean aomba raia kuwa makini,  wakitowa malalamiko kuhusu hali ya bwizi ndani ya kati.  Akiomba pia raia kwa jumla kujihusisha na maendeleo ya mahali.

Pamoja na hayo, viongozi wa jimbo kuwaunga mkono kwa kuwa wenyewe peke hawataweza.

Juvénal Murhula.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire