Akieleza kuhusu ziara yake mjini Kinshasa, Prezidenti wa soko ya Nguba pia Prezidenti wa muungano wa soko mjini Bukavu Étienne Buhendwa anena kuwa walijielekeza mjini Kinshasa ili kutanana na viongozi wa serkali. Ni katika lengo la kutafuta soko hizo zijengwe, katika kuheshimu kanuni za ujenzi wa soko za kimataifa.
Prezidenti wa soko ya Nguba alinena hayo, akihojiwa na mwana ripota wa la ronde info mjini Bukavu.
Ziara yangu ya kwenda Kinshasa ni ajili ya kwenda kutetea na kuomba hizi soko za mji ziwe miongoni mwa soko zenyi kuhesabilika, zijengwe kulingana na kanuni ya kimataifa. Sikukuwa mimi mwenyewe. Nilisindikizwa na Prezidenti wa shirika la raia mjini Bukavu pamoja naye Prezidenti makamu wa muungano wa soka mjini humo. Tulikutana viongozi kadhaa ; mfano waziri wa taifa husika n’a bajeti Aimé Bodji Sangara, ambaye tulipelekea malalamiko yetu. Tulikutana pia Kiongozi wa Cadeco nchini, ila hatujakomesha, aeleza Prezidenti wa soko ya Nguba.
Huyu akiongeza kwamba walitowa buku lao la malalamiko, ambalo waliahidi kulifikisha kwa wahusika. Wanabunge wa taifa wazaliwa wa Kivu ya kusini wakifahamishwa kuhusu malalamiko yao,
Akihojiwa kuhusu kile kinachofanyika kwa kungojea misaada mikubwa, Étienne Buhendwa anena yafwatayo:
<<Ukienda mtaani Kadutu, utakuta kwamba kuna kazi kubwa inayofanyika eneo hilo. Hiyo ni miongoni mwa kazi zetu, kwa kuwa Mheshimiwa Aimé Bodji aligusa ndani ya mfuko, na
kuanza ujenzi wa vyoo. Mwenyewe akitowa mabati zaidi ya 1000. Pamoja na hayo, tulipeleka malalamiko yetu kwa baba wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi, ambaye aliahidi suluhisho siku za usoni. Akifwatilia swala kwa makini,>> anena Prezidenti wa muungano wa soko mjini Bukavu Étienne Buhendwa.
Kwake Étienne, hakuna kazi ya kudumu yoyote ambayo imekwisha fanyika kuhusu ujenzi wa soko. Hata kama kiongozi wa mtaa anatumika bega kwa bega na kamati za soko mjini. Kwamba kazi inayofanyika ni ya dharura, kwa kungojea mkono wa liwali wa jimbo na serkali ya Kinshasa.
Étienne Buhendwa aomba raia kuunga mkono Raisi wa taifa Félix Antoine Tshisekedi, ili kazi alizozianza zipate kutekelezwa. Yote kupitia mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Akitowa mfano wa soko kubwa aliyoiona mjini Kinshasa ikijengwa vilivyo, wakati wa ziara yake.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.