Goma: Mzalendo mkuu Muhindo Nzangi aomba raia mjini Goma waweze kumcagua yeye na Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI ili watekeleze kazi walizozianza

Aliyekuwa waziri husika na yunivasti nchini DRC Muhindo Nzangi Butondo mwenyekiti wa chama cha kisiasa AVRP, ameomba raia mjini Goma kuweza kumcagua, kutokana na kazi alizozifanya alipokuwa bungeni na hata wakati huu kama waziri. Yeye akiwa nambari 83, ameomba raia waweze kuchaguwa pia Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI kwa kuwa ni moja wa ma Raisi wasio na woga wenyi kutumikia raia akiwa nambari 20.

Alitamka hayo mjini Goma wakati wa kuanzisha rasmi kampeni ya uchaguzi, akitokea mjini Kinshasa. Ilikuwa mbele ya umati uliomungojea kwa hamu kumlaki.

Katika hotuba yake, kandideti kwenyi bunge la taifa nambari 83 Mzalendo Muhindo Nzangi Butondo aligusia kazi kubwa alizozifanya bungeni, miongoni kupiganisha watu wenyi nia mbaya waliotaka Minembwe huko Kivu ya kusini igawanyike kama mtaa, wakiwa na nia mbaya ya kugawanya DRC. Wakati wote Muhindo Nzangi Butondo nambari 83 alitowa kauli akitetea raia walio mutuma kazini. Kuwa shujaa lilipelekeya atajwe naye Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI kuongoza wizara husika na yunivasti nchini DRC. Akifanya kazi mbali mbali wakati wa uongozi.

<Hapo mbeleni tulikuwa tukisoma miaka tano ili kupata cheti cha mwisho yaani licence kwa lugha la kimombo. Nilipochukuwa madaraka, nilifanya iwe miaka tatu ili kupata cheti katika mpango LMD kwa kimombo sawa na nchi jirani Na hiyo itapelekea wapate kazi baada ya mafunzo mafipi. Nikijihusisha pia na ujenzi wa shule, mfano ya jumba kinyumba ambayo ina sura nzuri, ISC na zingine nyingi nchini DRC. Pamoja na hayo niliendelea kukerwa na gisi nchi jirani zinaendelea kuvamia DRC. Pamoja na Raisi, niliona umuhimu vijana wafunzwe kazi ya jeshi mbele waendelee na mafunzo mengine kwenyi yunivasti. Kwa sasa maelfu ya wanachuo kutoka Kivu ya kaskazini, Kisangani tayari wamehitimisha mafunzo ya jeshi, ili kuwa tayari kupigania nchi. Pia nililazimisha vijana wafunzwe kiini kampyuta, ili waboreshe kazi zao na mengineo>>, akifasiria Mzalendo Muhindo Nzangi Butondo mwenyi kiti wa AVRP mbele ya umati.

Huyu alihitimisha hotuba yake akisisitiza raia wamuunge mkono wakichagua pia Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI ambaye ni nambari 20. Akisema kwamba Raisi ana moyo wa kutumikia raia, kwa kutekeleza usalama, maendeleo, uchumi na mengineo. Mzalendo Muhindo Nzangi Butondo nambari 83, alionyesha kwamba DRC imepata Raisi wa kweli, ambaye hana woga. Anayetaja kwa sauti kwamba DRC inashambuliwa na nchi ya Rwanda, jambo ambalo Raisi wengine waliogopa kutamka. Raisi ambaye amekubali vita kinaganaga na nchi jirani, akiwa na nia ya ushindi. Mzalendo mkuu Muhindo Nzangi Butondo akisema kwamba ni muda pia wa kuondowa kazini watumishi wa serkali wenyi, kutumika wakiwa na mguu moja nchini DRC na mwengine nchini Rwanda.

Baadae alionyesha mbele ya umati wazalendo wengine kandideti wa chama chake AVRP, miongoni mwao wakandideti kwenyi bunge la taifa, kwenyi bunge la jimbo, na hata washauri wa mitaa.

Juvénal Murhula..

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire