Siku chache baada ya kuondoka jimboni Kivu ya kaskazini na huko Ituri ili kujioneya hali ilioko kupitia uongozi wa kijeshi yaani état de siège, serkali ya DRC pamoja na mabunge wa taifa walikutana hii ijumaa tarehe 6 disemba, ili kucunguza mbele ripoti ilioko kabla ya kuipeleka kwake Raisi wa taifa.
Waziri mkuu Judith Suminwa Tuluka anena kwamba pendekezo zote, yaani za viongozi wa serkali wa mahali, za shirika la raia na hata zile za miungano kadhaa zilichukuliwa, wakionyesha kazi iliyofanyika na uongozi wa dharura.
Serkali pamoja na wanabunge, moja kwa moja walitowa maoni yao mbele ya kuipeleka ripoti kwake Raisi wa taifa, Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye ataamua kuhusu kubaki ama kuondoka kwa uongozi wa kijeshi, ama kugeuza.
Serkali ina lenga kujibu kwa matakwa ya raia kuhusu amani na usalama makwao. Kwa machache katika kikao hicho, walikubaliana kuhusu azimio ambazo zitatolewa kwake Raisi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
Tufahamishe kwamba wanabunge wa taifa kwa jumla wanena kutoona mara tena shabaa ya kuendelea na uongozi wa dharura yaani état de siège, ambao miaka tatu sasa bila matokeo bora.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.