Goma: Marie NYOMBO ZAINA anena kwamba atapigania haki ya mwanamke hadi mwisho

Mratibu wa shirika husika na kupigania haki ya mwanamke nchini DRC RENADEF Bi Marie NYOMBO

Mratibu wa shirika husika na maendeleo ya mwanamke nchini DRC Bi Marie NYOMBO ZAINA anena kuanzishwa kwa shirika lake lisilo la kiserkali RENADEF tangu mwaka 2002 wakati wa mripuko wa volkeno iliyo sababisha maafa mengi mjini Goma. Akitumika bega kwa bega na mashirika za kimataifa zilizojiri ajili ya misaada ya zarura kwa wahanga wa volkeno. Mashirika zilipofunga milango aliendelea na mradi ya kudumu.

Marie NYOMBO anena hayo baada ya kushiriki kwa siku ya kwanza ndani ya kikao kilichoandaliwa hii juma tatu tarehe 13 disemba 2021 ,na Muungano wa shirika husika na kupiganisha ukimwi CIELS kwa maarufu kipindi chake chake cha sita mjini Goma.

« Watu wote waliyahama maskani yao. Hata mimi nilikimbia huko Gisenyi nchini Rwanda baadae nikarudi ili kutumika na watu waliobaki mjini. Sisi kama wahusika na maendeleo na watetezi wa haki za binaadam tulianza kazi baada ya misaada yazarura. Tulikarabati hospitali kadhaa vijijini, kukabizi mikopo midogo kwa akina mama pia kilimo » anena akina mama huyu.

Mratibu nchini wa RENADEF aeleza kuwa shirika lake lahusika ndani ya sekta kadhaa yaani, haki ya binaadam, uchaguzi, kuinua mwanamke, mafunzo kuhusu uongozi wa mwanamke, mwanamke na afya, mazingira, mwanamke na maendeleo vijijini, ukingo wa watoto, kujitegemea kwa mwanamke. Bi Marie aongeza kuwa kutakuwa uhusiano kati ya shirika lake na kazi za akina mama ndani ya shirika zingine.

Akina mama huyu asema kufurahishwa na ripoti za kazi walizozitekeleza mwanzoni mwa shirika lao hadi sasa katika kupigania mwanamke, na nini iliyotekelezwa kwa kufikia lengo.

Tufahamishe kwamba shirika RENADEF lipo na miaka zaidi ya kumi na nane hadi sasa na inaandaa miradi mengine kwa mwaka 2022.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire